Mwanaume mmoja nchini Marekani ambaye ametumia zaidi ya miongo minne akisubiri kunyongwa ameachiwa kwa dhamana baada ya uchunguzi mpya wa vinasaba (DNA) kubaini kuwa ushahidi uliopatikana eneo la mauaji hauhusiani naye.
Douglas Stewart Carter mwenye umri wa miaka 71 alikuwa amehukumiwa kwa mauaji ya Eva Olesen yaliyotokea mwaka 1985 katika jimbo la Utah. Hata hivyo, mahakama sasa imeamuru aachiliwe kwa muda wakati akisubiri kusikilizwa upya kwa kesi hiyo.
Eva Olesen aliuawa kikatili nyumbani kwake baada ya kuchomwa kisu mara kadhaa na baadaye kupigwa risasi kichwani.

Uchunguzi mpya wa DNA uliofanyika hivi karibuni umeonyesha kuwa damu iliyopatikana kwenye kitasa cha mlango pamoja na vinasaba vilivyopatikana kwenye mpini wa kisu kinachodhaniwa kutumika katika mauaji hayo havilingani na Carter.
Ripoti zinaonyesha kuwa wakati wa kesi ya awali hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kimwili uliomhusisha Carter na eneo la tukio.

Hukumu yake ilitegemea zaidi maungamo aliyodai alilazimishwa kuyatoa pamoja na ushahidi wa mashahidi wawili waliodai aliwahi kujisifu kuhusika na mauaji hayo. Baadaye mashahidi hao walibadili kauli zao.
Carter amekuwa akisisitiza kwa miaka yote kuwa hana hatia na kwamba alisaini maungamo hayo baada ya kutishwa na maafisa wa polisi.
Hatua ya kuachiwa kwake imekuja baada ya mapambano marefu ya kisheria. Mwaka uliopita, Mahakama Kuu ya Utah iliamuru kesi hiyo isikilizwe upya baada ya kubaini kile ilichokiita matukio kadhaa ya makusudi ya ukiukwaji wa taratibu na wachunguzi wa kesi hiyo.Jaji Derek Pullan alisema ushahidi mpya wa DNA umeifanya kesi dhidi ya Carter kuwa dhaifu zaidi, ingawa bado mahakama inaona suala hilo linapaswa kuamuliwa kupitia usikilizwaji mpya wa kesi.
Baada ya kutoka gerezani, Carter atalazimika kuvaa kifaa cha kufuatilia mienendo yake kwa njia ya GPS huku akikaa karibu na familia ya mwanawe, Tyler Anger.
Wakili wake Neal Hamilton amesema mteja wake atahitaji msaada wa kisaikolojia ili kuhimili athari za miaka mingi aliyotumia gerezani akisubiri hukumu ya kifo.
Kwa upande mwingine, familia ya marehemu Eva Olesen imeeleza kutoridhishwa na kuachiwa kwa Carter, ikisema matokeo ya DNA pekee hayaondoi uwezekano wa kuhusika kwake katika tukio hilo.
Kesi hiyo ilipata sura mpya mwaka 2011 baada ya mashahidi wawili wa awali kupatikana nchini Mexico na kudai walishinikizwa kutoa ushahidi dhidi ya Carter. Walidai pia walipokea zawadi na fedha kutoka kwa polisi na kutishiwa kufukuzwa nchini ikiwa wasingemhusisha na mauaji hayo.
Ingawa matokeo mapya ya DNA yamemwondoa Carter katika ushahidi uliopatikana eneo la tukio, bado hayajabaini ni nani hasa aliyemuua Eva Olesen. Hivyo, Carter anatarajiwa kurejea mahakamani katika kesi mpya itakayotoa uamuzi mwingine kuhusu hatima yake baada ya miaka 41 ya kusubiri hukumu ya kifo.

Post a Comment