Marekani na Iran zimetangaza makubaliano mapya ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili ili kutoa nafasi ya mazungumzo ya amani na kuzuia mfumulizo wa mashambulizi mapya katika ukanda wa Ghuba. Tangazo hili limetolewa leo baada ya siku kadhaa za mvutano mkali.
Katika Kisiwa cha Lavan nchini Iran, kampuni ya kusafisha mafuta ya serikali ya Iran (NIORDC) imetangaza kuwa kituo chake cha kusafishia mafuta kimeshambuliwa kwa makombora yanayodaiwa kutoka kwa Marekani.
Iran imejibu shambulizi hilo kwa nguvu kwa kutuma droni na makombora katika anga la nchi za Kuwait na Falme za Kiarabu (UAE).
Katika Kisiwa cha Lavan nchini Iran, kampuni ya kusafisha mafuta ya serikali ya Iran (NIORDC) imetangaza kuwa kituo chake cha kusafishia mafuta kimeshambuliwa kwa makombora yanayodaiwa kutoka kwa Marekani.
Shambulizi hilo limefanyika hivi karibuni na limeathiri moja ya vituo muhimu vya kusindika mafuta nchini Iran.
Jeshi la Kuwait limekiri kwamba limekabiliana na droni 28 za Iran kati ya saa 2 asubuhi na saa 7 mchana.
Baadhi ya droni hizo ziliripotiwa kulenga mitambo muhimu ya mafuta na vituo vya kuzalisha umeme kusini mwa Kuwait.
Aidha, jeshi la ulinzi wa anga la Falme za Kiarabu (UAE) limesema lilishambuliwa na “kitisho cha kombora” mnamo saa 7:30 mchana. Taarifa hiyo ilitolewa baada ya mifumo yao ya ulinzi kugundua vitisho vinavyotoka upande wa Iran.
Ikumbukwe kwamba Rais wa Marekani, Donald Trump, alikuwa ameahidi kuhirisha mashambulizi yaliyopangwa dhidi ya vituo vya nishati nchini Iran kwa wiki mbili, ikiwa Iran itaruhusu upitaji huru wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz. Hata hivyo, mvutano umeendelea kushika kasi licha ya ahadi hiyo.
Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limethibitisha kusitisha vita, lakini limesisitiza kuwa mapendekezo ya amani yanayojadiliwa ni lazima yahusishe “Iran kuendelea kuwa na mamlaka juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz.”

Hii inaonyesha kuwa Iran haitakubali kutoa udhibiti wake katika njia muhimu ya biashara ya mafuta duniani.
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, ambaye amekuwa mpatanishi mkuu katika mgogoro huu, amethibitisha kuwa nchi yake inaendelea kufanya kazi na pande zote mbili ili kuleta utulivu na mazungumzo yenye tija.

Sharif amesisitiza umuhimu wa diplomasia ili kuepuka vita kamili katika eneo la Ghuba ambalo linaweza kuathiri uchumi wa dunia kwa ujumla.
Mgogoro huu umeongeza wasiwasi mkubwa kimataifa, kwani Mlango-Bahari wa Hormuz ni njia muhimu ambapo zaidi ya theluthi moja ya mafuta ya dunia hupitia.

Wataalamu wanaonya kwamba ikiwa mapigano yataendelea, bei ya mafuta inaweza kupanda sana na kusababisha msukosuko wa kiuchumi duniani kote.
Hadi sasa, pande zote mbili zinaonekana kuwa makini na makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda, ingawa imani bado ni ndogo kutokana na historia ya mvutano kati ya Marekani na Iran.

Mazungumzo ya amani yanatarajiwa kuanza hivi karibuni chini ya usimamizi wa nchi kadhaa zinazotajwa kuwa na upande wowote
Post a Comment