Jeshi la polisi Latoa Tamko hili Kwa wananchi watakaohudhuria kesi ya Tundu lisu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza masikitiko yake kufuatia taarifa zinazodai kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linajiandaa kuchukua hatua kali za kiusalama dhidi ya wananchi watakaofika katika Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam mnamo Juni 11, 2026, kufuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho, kumekuwa na madai kwamba polisi wamepokea taarifa za kiintelijensia zinazoeleza kuwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA wanapanga kufanya vurugu katika eneo la mahakama. 

Inadaiwa kuwa kutokana na taarifa hizo, jeshi hilo limeweka mikakati maalum ya kuimarisha ulinzi na usalama, jambo ambalo limezua hofu miongoni mwa wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Hata hivyo, CHADEMA imekanusha vikali madai hayo na kusisitiza kuwa hakuna mpango wowote wa kufanya vurugu au kuvuruga amani wakati wa shughuli za mahakama. 

Chama hicho kimeeleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na zimekusudiwa kuchafua taswira yake mbele ya wananchi pamoja na kuhalalisha matumizi ya nguvu dhidi ya watu wanaotaka kufuatilia kesi hiyo kwa njia za amani.

Post a Comment

Previous Post Next Post