Uganda inaendelea kushuhudia hali ya mvutano mkubwa kisiasa, huku kiongozi wa upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, akitoa malalamiko makali dhidi ya serikali ya Rais Yoweri Museveni.
Kwa sasa, ni wazi kwamba hali hii itaendelea kuathiri siasa, usalama, na hali ya kijamii nchini Uganda. Wadau wa siasa za Afrika Mashariki wanaendelea kufuatilia kwa makini, kwani mzozo huu unaweza kuwa na athari kubwa kwa amani na utulivu wa kanda.
Bobi Wine amedai kwamba zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha katika kipindi cha wiki moja tu, akiwashutumu wanajeshi na Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais na Mkuu wa Majeshi ya Uganda, kwa kushirikiana na ukandamizaji huu.
Kupitia taarifa yake kwenye mtandao wa X, Bobi Wine alisema kuwa Muhoozi alionekana kufurahishwa na kifo cha wafuasi wake 22, lakini idadi halisi ni kubwa zaidi, ikifikia zaidi ya 100.
Kupitia taarifa yake kwenye mtandao wa X, Bobi Wine alisema kuwa Muhoozi alionekana kufurahishwa na kifo cha wafuasi wake 22, lakini idadi halisi ni kubwa zaidi, ikifikia zaidi ya 100.
Kauli hii inakuja baada ya matamshi ya Muhoozi yaliyoashiria vitisho kwa Bobi Wine, jambo lililochochea hofu kubwa miongoni mwa wafuasi wake.
Hali ya kisiasa nchini Uganda imekuwa tete. Bobi Wine amekiri kwamba amejificha nyumbani kwake baada ya polisi kufanya uvamizi.
Hali ya kisiasa nchini Uganda imekuwa tete. Bobi Wine amekiri kwamba amejificha nyumbani kwake baada ya polisi kufanya uvamizi.
Wanajeshi walisema kuwa nyumba yake imezingirwa na waliagiza wanaume wote waondoke, hali iliyoongeza hofu kuhusu usalama wa kiongozi huyo wa upinzani.
Aidha, Jenerali Muhoozi alimpa Bobi Wine saa 48 kujisalimisha kwa polisi, hatua iliyochukuliwa kama presha kubwa ya kisiasa dhidi yake.
Polisi wa Uganda wamesema Bobi Wine bado anapatikana nyumbani, lakini amekataa kuruhusu wanahabari kumtembelea.
Polisi wa Uganda wamesema Bobi Wine bado anapatikana nyumbani, lakini amekataa kuruhusu wanahabari kumtembelea.
Taarifa kutoka vyanzo vinavyomkaribia zinaonyesha kwamba hali ya usalama kwa upande wa upinzani inazidi kuwa mbaya, huku vitisho vya kifo vinavyokabili viongozi wa upinzani vikiongezeka.
Uganda ina historia ndefu ya ukandamizaji wa kisiasa, ambapo serikali ya Museveni imekuwa ikitumia vyombo vya dola kushinikiza upinzani na kuwanyima haki za kimsingi za kutoa mawazo.
Uganda ina historia ndefu ya ukandamizaji wa kisiasa, ambapo serikali ya Museveni imekuwa ikitumia vyombo vya dola kushinikiza upinzani na kuwanyima haki za kimsingi za kutoa mawazo.
Hali hii ya sasa inachukuliwa kuwa mbaya zaidi, kwani mauaji na vitisho vinavyoendelea vinaashiria hatari kwa mustakabali wa siasa nchini.
Bobi Wine, ambaye pia ni msanii maarufu, amejitokeza kama kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa, hasa miongoni mwa vijana.
Bobi Wine, ambaye pia ni msanii maarufu, amejitokeza kama kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa, hasa miongoni mwa vijana.
Hata hivyo, licha ya umaarufu wake, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka serikalini, hali inayonyesha jinsi mvutano wa kisiasa unavyokuwa mkubwa nchini Uganda.

Post a Comment