Jeshi la Marekani Laingia Katika Magumu Baada ya Taarifa Hii Mbaya Kutokea, Kwakweli Vita ni Mbaya!

TEHRAN, IRAN — Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limetoa tamko kali likidai kuwa limefanikiwa kuvunja kile walichokiita “kiburi” cha Rais wa Marekani Donald Trump katika mzozo unaoendelea wa kijeshi katika ukanda wa Asia Magharibi. 

Kupitia operesheni mpya waliyoipa jina la “Ahadi ya Kweli Namba Nne” (True Promise 4), Iran inasisitiza kuwa vikosi vya Marekani sasa vinakabiliwa na hali ngumu na haviwezi kuzuia mashambulizi ya Jamhuri hiyo.

Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Iran, Brigadia Jenerali Abfaz Sheekarchi, amesema operesheni hiyo ni jibu la moja kwa moja kwa mashambulizi yaliyofanyika tarehe 28 Februari ambayo Iran inadai yalifanywa na Marekani kwa kushirikiana na Israel. 

Mashambulizi hayo yalitajwa na Tehran kuwa chanzo cha kuanza kwa wimbi jipya la mapambano katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya IRGC, katika operesheni hiyo Iran imetumia makombora ya kisasa ikiwemo makombora ya Fattah yanayotajwa kuwa na kasi ya hypersonic pamoja na makombora ya Kheibar na Khorramshahr, ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vikubwa vya milipuko na kupiga malengo kwa umbali mrefu.

Jenerali Sheekarchi pia amemkosoa vikali Rais Donald Trump akimtaja kama kiongozi anayetoa madai yasiyoendana na hali halisi ya vita. 

Amesema madai ya Marekani kwamba imeharibu mifumo ya ulinzi ya Iran ni propaganda zinazolenga kupunguza morali ya wananchi wa Iran na kuonyesha ushindi ambao haupo.

Katika kauli yake, Sheekarchi alidai kuwa Marekani imeanzisha mashambulizi ili kulinda maslahi ya Israel katika eneo hilo, lakini sasa vikosi vya Marekani vinakabiliwa na upinzani mkali kutoka Iran na washirika wake katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Taarifa kutoka Tehran zinaeleza kuwa mashambulizi ya hivi karibuni yamelenga maeneo yanayodaiwa kuwa na maslahi ya kijeshi ya Marekani pamoja na vituo vya mawasiliano katika Israel. 

Iran pia imesema imeimarisha uwezo wake wa kijeshi katika Bahari ya Ghuba na karibu na Mlango Bahari wa Hormuz.

Mamlaka za Iran zimeendelea kusisitiza kuwa hakuna eneo lenye maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati ambalo liko salama iwapo mashambulizi dhidi ya Iran yataendelea. 

Kauli hiyo imeongeza hofu ya kuongezeka kwa mvutano katika eneo hilo muhimu kwa usafirishaji wa nishati duniani.

Katika hitimisho la tamko lake, IRGC imesema Iran haitarudi nyuma licha ya vitisho kutoka Washington. 

Jeshi hilo linadai bado lina akiba kubwa ya silaha za kisasa ambazo zinaweza kutumika katika hatua nyingine za mapambano iwapo hali ya vita itaendelea.

Post a Comment

Previous Post Next Post