Rais wa Marekani Donald Trump ameripotiwa kutoa maagizo ya kusitishwa kwa mashambulizi yaliyokuwa yakielekezwa dhidi ya Iran, hatua ambayo imeibua mjadala mkubwa kuhusu mwelekeo wa mgogoro huo na mustakabali wa usalama katika Mashariki ya Kati.
Uamuzi huo unatajwa kuja wakati juhudi za kidiplomasia zinazosimamiwa na Oman zikionyesha dalili za maendeleo, huku kukiwa na matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano yatakayosaidia kupunguza mvutano na kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, eneo muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani. SOMA ZAIDI.
Post a Comment