Kamanda Wa Jeshi La Marekani Atoa Onyo Kali Kwa Trump Adai Hakuna Faida Yeyote Ya Kuishambulia Iran

Kamanda wa Jeshi la Marekani katika Kanda ya Mashariki ya Kati (CENTCOM), Jenerali Brad Cooper, ameripotiwa kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa Marekani kuchukua hatua zaidi za kijeshi dhidi ya Iran, akieleza kuwa uvamizi wa moja kwa moja unaweza kuhitaji rasilimali kubwa za kijeshi na kuwa na gharama kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Jenerali Cooper amependekeza kusitishwa kwa kampeni ya mashambulizi ya anga inayolenga maeneo yanayohusishwa na shughuli za kijeshi za Iran katika eneo la Mlango wa Bahari wa Hormuz, akidai kuwa operesheni hiyo imefikia hatua ambayo kuendelea nayo huenda kusitoe mafanikio makubwa ya ziada bila Marekani kuingia katika awamu mpya ya vita vya kiwango kikubwa.SOMA ZAIDI.

Post a Comment

Previous Post Next Post