Kesi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeendelea tena leo Februari 9, 2026 huku hoja mpya zikijitokeza mahakamani kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki zake akiwa mahabusu.
Kikao hicho kilivuta hisia za watu wengi waliohudhuria, ambapo baadhi ya wananchi walionekana kuonyesha hisia zao wazi mara tu alipowasili ndani ya ukumbi wa Mahakama.
Lissu aliingia akiwa amevaa mavazi ya kaki na kubeba nyaraka pamoja na vitabu kadhaa, akionekana mwenye utulivu na kujiamini.

Baada ya Majaji kuketi, karani alisoma namba ya shauri na upande wa Jamhuri ukawakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali akishirikiana na mawakili wengine wa Serikali.
Upande wa mashtaka ulieleza kuwa uko tayari kuendelea na mwenendo wa kesi mara tu mshitakiwa atakapokuwa tayari kuwasilisha hoja zake.
Alipopatiwa nafasi ya kuzungumza, Lissu alianza kwa kutoa salamu za Mwaka Mpya kwa Mahakama na mawakili waliokuwepo kabla ya kuelekeza hoja zake katika masuala anayodai yanakiuka haki zake za kisheria akiwa gerezani.

Alisisitiza kuwa Majaji wana wajibu wa kusimamia haki za wafungwa kwa mujibu wa sheria za magereza, akirejea vifungu mbalimbali vinavyohusu haki za mahabusu kuwasilisha malalamiko yao mbele ya Mahakama.
Hoja yake ya kwanza ilijikita kwenye haki ya kuwasiliana na mawakili wake kwa faragha. Alidai kuwa kumekuwa na tabia ya maafisa wa magereza kukaa karibu na kusikiliza mazungumzo yake na mawakili, jambo alilosema linakiuka kanuni za usimamizi wa magereza zinazolinda mawasiliano ya kisheria.

Kwa mujibu wa maelezo yake, hali hiyo ilianza tangu alipokuwa katika Gereza la Kisutu na imeendelea hadi sasa, jambo analoamini linadhoofisha maandalizi yake ya kujitetea mahakamani.
Upande wa Serikali kupitia wakili mmoja ulisimama na kuomba mwongozo wa Mahakama kuhusu pingamizi lililowasilishwa awali, lakini Lissu alieleza kuwa hakuwasilisha ombi rasmi bali alikuwa anatoa taarifa ili iingizwe kwenye rekodi za Mahakama, akisisitiza kuwa ni jukumu la Majaji kuamua hatua stahiki.
Akiendelea na maelezo yake, alidai kuwa tangu Novemba 2025 utaratibu wa kukutana na mawakili wake ulibadilika, ambapo sasa hukutana katika ofisi ya usalama wa gereza akiwa amezungukwa na maafisa kadhaa.

Alisema kwa kipindi kirefu mazungumzo yake yamekuwa yakisikilizwa na kila anapouliza sababu huambiwa kuwa ni “maagizo kutoka juu,” kauli aliyodai inahitaji ufafanuzi wa kisheria.
Hoja ya pili aliyowasilisha ilihusu haki ya kupokea wageni wasiokuwa ndugu wa karibu au mawakili, akisema kanuni za magereza zinatoa nafasi hiyo chini ya masharti maalum.

Alidai kuwa vikwazo vilivyowekwa vinakiuka haki hiyo na vinaathiri uwezo wake wa kuwasiliana na wadau wengine muhimu.
Post a Comment