Bunge la Umoja wa Ulaya (European Parliament) na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (European Commission) zimeingia katika Mjadala mkubwa kuhusu mpango wa kuipatia Tanzania msaada wa kimaendeleo wa kiasi cha Euro Milioni 156 (zaidi ya Tsh. Bilioni 440).
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida la Euractiv Juni 3 2026, Wabunge wa Ulaya wameungana kupinga vikali kutolewa kwa fedha hizo kwa sasa Wakiituhumu Kamisheni ya Ulaya kwa kutaka kutoa fedha hizo bila kuweka masharti madhubuti ya kulinda haki za binadamu.
Mambo Muhimu Yaliyojitokeza Kwenye Sakata Hili:
Vurugu na Vifo vya Baada ya Uchaguzi (Oktoba 2025): Wabunge wa EU wameibua hoja nzito kuhusu ukandamizaji wa maandamano kufuatia uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2025. Kwenye taarifa yao, wanadai kuwa zaidi ya watu 500 walipoteza maisha kwenye vurugu hizo.
Kufungwa kwa Tundu Lissu: Bunge hilo limehoji kuendelea kuswekwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu.

Wabunge hawa (wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, David McAllister) wanadai mashtaka anayokabiliwa nayo ni ya kisiasa.
Post a Comment