Wakati Tanzania ikiendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa baadhi ya maeneo bado yanakabiliwa na changamoto kubwa ya maambukizi.
Kwa mujibu wa matokeo ya Utafiti wa Athari za VVU Tanzania (THIS) wa mwaka 2022/2023, mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe na Ruvuma ndiyo inayoongoza kwa viwango vya juu vya maambukizi ya VVU nchini.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa asilimia 12.7 ya maambukizi, ukifuatiwa na Iringa wenye asilimia 11.1, Mbeya asilimia 9.6, Songwe asilimia 7.1 na Ruvuma asilimia 4.5. Hali hii imeibua maswali mengi kuhusu sababu zinazofanya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuendelea kuwa na viwango vya juu vya maambukizi ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.
Moja ya sababu kuu zinazotajwa ni historia ndefu ya maambukizi katika ukanda huo. Kwa miaka mingi, mikoa hiyo imekuwa ikiripoti idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU.

Hii ina maana kuwa uwezekano wa maambukizi mapya kuendelea kutokea huwa mkubwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo tayari na virusi hivyo.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kadiri idadi ya watu wanaoishi na VVU inavyokuwa kubwa katika eneo fulani, ndivyo hatari ya maambukizi mapya inavyoongezeka ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa. SOMA ZAIDI.
Post a Comment