Iran Yaingia Katika Magumu Baada ya Taarifa Hii Mbaya Kutokea

Mvutano kati ya Iran na Israel umeingia katika hatua nyingine ya tahadhari kubwa baada ya Iran kudai kuwa imefanikiwa kuidungua ndege ya kijasusi ya Israel katika anga la jimbo la Hormozgan kusini mwa nchi hiyo.....TAZAMA VIDEO HAPA.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, ndege hiyo aina ya “Orbiter” ilikuwa ikifanya shughuli za upelelezi kabla ya kushambuliwa na mifumo maalumu ya ulinzi wa anga ya Iran. Mabaki ya ndege hiyo yameripotiwa kupatikana kwa ushirikiano wa vikosi vya majini vya Iran katika eneo hilo.

Maafisa wa kijeshi wa Iran wamesema ndege hiyo ilikuwa na uwezo wa kukwepa rada, lakini walisisitiza kuwa teknolojia yao mpya ya ulinzi imeweza kuigundua na kuiteketeza kabla haijatekeleza jukumu lake kikamilifu. 

Iran imeeleza kuwa mfumo uliotumika bado ni siri ya kijeshi, jambo ambalo limeongeza mijadala kuhusu uwezo mpya wa Tehran katika vita vya kisasa vya anga.

Hadi sasa, Israel haijatoa tamko rasmi linalothibitisha au kukanusha tukio hilo, ingawa baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa jeshi lao halijafahamu kwa undani madai hayo ya Iran. 

Hali hiyo imeacha maswali mengi kuhusu ukweli wa tukio hilo na athari zake katika mvutano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Post a Comment

Previous Post Next Post