Beirut, Juni 2026 — Hali ya usalama kati ya Lebanon na Israel imeendelea kuwa tete baada ya ripoti kusambaa zikidai kuwa ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Israel aina ya Elbit Hermes 450 ilidunguliwa katika Bonde la Bekaa magharibi mwa Lebanon, tukio ambalo limeongeza hofu ya kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka eneo la tukio, ndege hiyo ilikuwa katika operesheni ya upelelezi wa kijeshi kabla ya kudaiwa kulengwa na kombora la ulinzi wa anga lililorushwa kutoka ardhini.
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka eneo la tukio, ndege hiyo ilikuwa katika operesheni ya upelelezi wa kijeshi kabla ya kudaiwa kulengwa na kombora la ulinzi wa anga lililorushwa kutoka ardhini.
Baada ya kushambuliwa, drone hiyo iliripotiwa kuanguka katika eneo hilo, hali iliyosababisha uharibifu na kuibua tahadhari mpya kuhusu matumizi ya teknolojia ya kijeshi angani katika maeneo yenye migogoro.
Post a Comment