Serikali kupitia Wizara ya Fedha imetangaza kuanza rasmi kwa Awamu ya Pili ya zoezi la uhakiki binafsi kwa wastaafu wote wanaolipwa pensheni kupitia Hazina..................TAZAMA VIDEO.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa malipo ya pensheni, kuongeza uwazi katika mfumo wa malipo na kuhakikisha fedha za umma zinawafikia walengwa halali kwa wakati unaotakiwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha, zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 1 Juni hadi 15 Julai 2026 na linawahusu wanufaika wote waliopo katika Daftari la Pensheni la Hazina ambao hawakufanikiwa kujihakiki katika awamu ya kwanza iliyokamilika mwezi Mei mwaka huu.

Serikali imeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya maboresho yanayoendelea kufanywa katika mfumo wa usimamizi wa pensheni nchini.
Makundi yanayohusika katika awamu hii ni pamoja na wastaafu wanaolipwa pensheni ya kawaida kupitia Hazina, askari wanaopokea pensheni ya ulemavu pamoja na wajane na wagane wanaonufaika na malipo ya pensheni kutoka serikalini.

Serikali imeweka msisitizo kwamba kila mnufaika ambaye hajakamilisha uhakiki wake anapaswa kufanya hivyo ndani ya muda uliopangwa ili kuepuka usumbufu katika malipo ya pensheni yake.
Post a Comment