Hali ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati imezidi kuwa tete kufuatia Iran kutekeleza shambulio kubwa la makombora dhidi ya mji wa Tel Aviv nchini Israel, yakidaiwa kuwa na vichwa vya milipuko vinavyosambaa, hatua inayotafsiriwa kama kulipiza kisasi kwa kuuawa kwa mkuu wake wa usalama, Ali Larijani.
Shambulio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatano limesababisha vifo vya watu wawili karibu na eneo lenye msongamano mkubwa wa watu pamoja na miundombinu ya kijeshi.
Wakati hali ikiwa bado inazidi kuwa mbaya, tukio jingine limeripotiwa nchini Iran ambapo kombora lilianguka karibu na kituo cha nyuklia cha Bushehr.
Shambulio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatano limesababisha vifo vya watu wawili karibu na eneo lenye msongamano mkubwa wa watu pamoja na miundombinu ya kijeshi.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, tukio hilo limeongeza idadi ya vifo nchini Israel kufikia takribani watu 14 tangu kuanza kwa mashambulizi hayo ya pande mbili.
Iran imeeleza kuwa ilitumia makombora ya kisasa aina ya Khorramshahr-4 pamoja na Qadr, ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vingi vya milipuko vinavyosambaa katika maeneo tofauti.

Kwa upande wake, Israel imekiri changamoto ya kuyazuia makombora ya aina hiyo, ikidai kuwa teknolojia hiyo inafanya ulinzi kuwa mgumu zaidi na kuongeza hatari kwa raia.
Ingawa halikusababisha madhara yoyote makubwa, tukio hilo limezua hofu ya uwezekano wa ajali ya nyuklia endapo mashambulizi yataendelea karibu na maeneo nyeti kama hayo.
Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limetoa tahadhari kali likionya juu ya hatari inayoweza kutokea iwapo miundombinu ya nyuklia itahusishwa moja kwa moja katika mapigano hayo.

Shirika hilo limesisitiza umuhimu wa pande zote kuchukua tahadhari ili kuepusha janga kubwa zaidi ambalo linaweza kuathiri si tu eneo hilo bali dunia nzima.
Mapigano kati ya Israel na Iran yanaendelea kushika kasi huku taarifa zikionyesha kuongezeka kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi pamoja na vifo vya viongozi waandamizi kutoka pande zote.

Hali hiyo imeifanya jamii ya kimataifa kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya uwezekano wa vita kamili vinavyoweza kuvuta mataifa mengine kujiingiza.
Juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano zinaonekana kukwama, huku taarifa zikidai kuwa uongozi mpya wa Iran haujaonyesha dalili za kukubali mazungumzo ya kusitisha mapigano kwa haraka.

Hali hii inaongeza hofu kwamba mzozo huo unaweza kuendelea kwa muda mrefu zaidi na kusababisha madhara makubwa kwa raia na uchumi wa eneo hilo.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaonya kuwa matumizi ya silaha zenye uwezo mkubwa kama makombora yenye vichwa vya milipuko vinavyosambaa yanaweza kubadilisha mwelekeo wa vita hivyo na kuongeza ukubwa wa uharibifu.

Aidha, wanasisitiza umuhimu wa hatua za haraka za kidiplomasia ili kuzuia hali hiyo isigeuke kuwa janga la kimataifa.
Kadri hali inavyoendelea kubadilika kwa kasi, macho ya dunia yanaendelea kuelekezwa katika eneo hilo, huku wengi wakisubiri kuona hatua zitakazochukuliwa na pande husika ili kudhibiti mzozo huo unaozidi kuwa hatari siku hadi siku.

Post a Comment