Angalau watu 400 wanaripotiwa kuuawa katika shambulio la anga lililolenga hospitali ya watumiaji wa dawa za kulevya.
Afghanistan imeinanga Pakistan kwa kuilenga hospitali hiyo katika mji mkuu wa Afghan, Kabul.
Tukio hilo limeashiria kuongezeka kwa kasi kwa mzozo ulioanza mwishoni mwa mwezi uliopita na umeshuhudia mapigano ya mara kwa mara ya mipakani pamoja na mashambulizi ya anga ndani ya Afghanistan.
Pakistan ilidai kuwa mashambulizi yake, ambayo pia yalifanyika mashariki mwa Afghanistan, hayakupiga maeneo yoyote ya kiraia na kukanusha shutuma za Afghanistan.
Naibu msemaji wa serikali ya Afghanistan, Hamdullah Fitrat, katika chapisho kwenye mtandao wa X, alisema shambulio hilo la anga liliipiga hospitali hiyo majira ya saa 3 usiku kwa saa za huko, na kuharibu sehemu kubwa ya kituo hicho chenye vitanda 2,000.
Alisema idadi ya vifo "hadi sasa" imefikia watu 400, huku wengine takriban 250 wakiripotiwa kujeruhiwa.
Picha zilizowekwa na vituo vya televisheni vya ndani kwenye mtandao wa X zilionyesha vikosi vya usalama vikitumia tochi wakati vikibeba majeruhi huku wazima moto wakihangaika kuzima moto katikati ya mabaki ya jengo.
Bw. Fitrat alisema timu za uokoaji zilikuwa zikifanya kazi kudhibiti moto na kuopoa miili.
Shambulio hilo limekuja saa chache baada ya maafisa wa Afghanistan kusema pande hizo mbili zilishambuliana kwa risasi kando ya mpaka wao wa pamoja, na kuua watu wanne nchini Afghanistan, huku mapigano hayo mabaya zaidi kati ya majirani hao katika kipindi cha miaka mingi yakiingia wiki ya tatu.
Msemaji wa serikali ya Afghanistan, Zabiullah Mujahid, alilaani shambulio hilo kupitia X, akiishutumu Pakistan kwa "kulenga hospitali na maeneo ya kiraia ili kufanya vitendo vya kutisha"
Katika chapisho kabla ya idadi ya vifo kupanda na kufikia mamia, alisema waliouawa na kujeruhiwa walikuwa wagonjwa katika hospitali hiyo.
"Tunalaani vikali uhalifu huu na tunachukulia kitendo kama hicho kuwa kinyume na kanuni zote zinazokubalika na ni uhalifu dhidi ya ubinadamu," alichapisha.
Msemaji wa Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, Mosharraf Zaidi, alitupilia mbali madai hayo akisema hayana msingi, akisema hakuna hospitali iliyolengwa huko Kabul.
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Wizara ya Habari ya Pakistan ilisema mashambulizi hayo "yalilenga kwa usahihi mitambo ya kijeshi na miundombinu ya kusaidia magaidi ikiwa ni pamoja na ghala la vifaa vya kiufundi na ghala la risasi la Taliban wa Afghanistan" na wanamgambo wa Pakistan wenye makazi yao Afghanistan huko Kabul na Nangarhar, ikisema vituo hivyo vilikuwa vikitumiwa dhidi ya raia wasio na hatia wa Pakistan.
Ilisema ulengaji wa Pakistan ulikuwa "wa usahihi na uliofanywa kwa uangalifu ili kuhakikisha hakuna uharibifu wa pembeni unaosababishwa".
Wizara hiyo ilisema dai la Bw. Mujahid lilikuwa "la uongo na la kupotosha" na lililenga kuchochea hisia na kufunika kile ilichokitaja kama "msaada haramu kwa ugaidi wa mipakani".
Shambulio hilo limekuja saa chache baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa wito kwa viongozi wa Taliban wa Afghanistan kuongeza juhudi mara moja za kupambana na ugaidi.
Pakistan inaishutumu Kabul kwa kuhifadhi makundi ya wanamgambo, hasa Taliban wa Pakistan, ambao inasema hufanya mashambulizi ndani ya Pakistan.
Azimio la Baraza la Usalama, lililopitishwa kwa kauli moja, halikuijata Pakistan lakini linalaani "kwa kauli kali zaidi shughuli zote za kigaidi ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya kigaidi".
Azimio hilo pia linaongeza muda wa ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Unama, kwa miezi mitatu.
Serikali ya Pakistan mara nyingi huishutumu serikali ya Taliban ya Afghanistan kwa kutoa hifadhi salama kwa Taliban wa Pakistan, ambao wameorodheshwa kama shirika la kigaidi na Marekani, pamoja na makundi haramu ya wanaotaka kujitenga wa Baloch na wanamgambo wengine ambao mara kwa mara hushambulia vikosi vya usalama vya Pakistan na raia kote nchini humo.

Post a Comment