Marekani imefanya mashambulizi mapya ya anga katika maeneo ya kusini mwa Iran, yakilenga mifumo ya makombora pamoja na meli zinazodaiwa kuhusika katika shughuli za uwekaji mabomu ya majini katika Mlango wa Hormuz. Hatua hiyo imeongeza hofu ya kuongezeka kwa mgogoro mkubwa wa kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Katika taarifa yake, Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema operesheni hiyo ilifanyika kama hatua ya “kujilinda” kwa lengo la kulinda wanajeshi wa Marekani pamoja na maslahi yake dhidi ya vitisho vinavyodaiwa kutoka kwa vikosi vya Iran.
Kwa mujibu wa CENTCOM, mashambulizi hayo yalilenga miundombinu ya makombora ya Iran pamoja na meli zilizoripotiwa kujaribu kuweka mabomu ya majini katika maeneo muhimu ya baharini.
Ripoti mbalimbali zimeeleza kuwa wanajeshi kadhaa wa Iran wamepoteza maisha katika mashambulizi hayo.

Marekani inaamini kuwa shughuli hizo zilikuwa tishio kubwa kwa usalama wa usafirishaji wa kimataifa kupitia Mlango wa Hormuz, ambao ni njia muhimu kwa biashara ya mafuta duniani.
Operesheni hiyo mpya imekuja wakati hofu ikiendelea kuongezeka kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa vita kubwa zaidi katika Mashariki ya Kati.

Wachambuzi wa masuala ya usalama wanaonya kuwa hatua za kijeshi kutoka pande zote zinaweza kuongeza mvutano na kusababisha mgogoro mkubwa wa kikanda.
Ripoti mbalimbali zimeeleza kuwa wanajeshi kadhaa wa Iran wamepoteza maisha katika mashambulizi hayo.
Wakati huo huo, Iran imedai kuwa imefanikiwa kudungua ndege mbili zisizo na rubani za Marekani aina ya MQ-9 Reaper ambazo zilikuwa zikifanya operesheni za upelelezi karibu na kambi ya kijeshi ya Bandar Abbas.
Tehran imeeleza kuwa ndege hizo zilikuwa zikikusanya taarifa za kijeshi katika eneo hilo na kwamba vikosi vya Iran vilichukua hatua za haraka kuzidungua kabla hazijatekeleza kikamilifu operesheni zao.

Hata hivyo, Marekani bado haijatoa taarifa rasmi kuthibitisha madai hayo ya Iran kuhusu kudunguliwa kwa ndege hizo.
Licha ya mashambulizi hayo, Marekani na Iran bado zinaendelea na mazungumzo yanayolenga kutafuta suluhisho la mgogoro unaoendelea kati ya mataifa hayo mawili pamoja na hali ya usalama katika Mashariki ya Kati.

Moja ya ajenda kuu katika mazungumzo hayo ni kufikiwa kwa makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Marekani imeendelea kusisitiza kuwa haitasita kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran au taifa lolote litakalohatarisha maisha ya raia wake au maslahi yake duniani.

Wachambuzi wa kimataifa wanaamini kuwa mashambulizi hayo ni ujumbe wa wazi kwamba Washington iko tayari kutumia nguvu kubwa kulinda ushawishi wake katika eneo hilo.
Kwa upande mwingine, Iran imeonya kuwa itajibu kwa nguvu mashambulizi yoyote yatakayolenga maeneo yake ya kijeshi au miundombinu yake muhimu.

Hali hiyo imeongeza tahadhari katika mataifa mengi huku dunia ikiendelea kufuatilia kwa karibu hatua zinazofuata kutoka Washington na Tehran.
Post a Comment