Iringa — Joto la kisiasa limezidi kupanda kufuatia ziara ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa, ambako ametoa ujumbe mzito kwa watendaji wa serikali waliotuhumiwa kupuuza kero za wananchi.
Kauli zake zimeibua mjadala mpana wa kisiasa na kiutawala, huku zikionekana kubeba msimamo mkali wa uwajibikaji kwa viongozi wa umma.
Katika hotuba yake, Dkt. Mwigulu alisisitiza kuwa watendaji wa serikali wanapaswa kubeba changamoto za wananchi kama sehemu ya majukumu yao ya kila siku, akionya tabia ya dharau na uzembe katika utoaji wa huduma.

Amesema wananchi ndio msingi wa uongozi, hivyo hakuna mtendaji anayepaswa kuonyesha kiburi au uzito katika kushughulikia matatizo yao.
Post a Comment