Sakata Polepole la Lafika Pazuri! Mtetezi Wake Utuma Ujumbe Huu Mzito Akikana Tuhuma Hizi

Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Wakili Boniface Mwabukusi, limeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu namna Tume ya kuchunguza matukio ya ghasia za Oktoba 29, 2025 inavyoshughulikia kisa hicho. 

Mwabukusi amesisitiza kuwa moja ya changamoto kubwa ni kutokutoa maelezo yanayothibitishwa kuhusu masuala nyeti, ikiwemo utekaji, upotevu wa watu akitolea mfano wa Humphrey Polepole na mauaji, na badala yake Tume imekuwa ikitegemea taarifa za vyombo vya dola bila kufanya uchunguzi huru.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya TLS jijini Dar es Salaam, Mei 11, 2026, Mwabukusi alisema, "Moja ya jambo hili ni kusema watu wamekufa, wapo mochwari halafu wakapotea. 

Tume inaishia hapo bila kufafanua au kwenda zaidi kutuambia nini kilijiri, nini kifanyike, walitokaje mochwari, nani alikuwepo mochwari? Hili ni eneo ambalo lilitakiwa lipewe majibu kwani kuna Watanzania ambao kufuatia ndugu zao kuuwawa, kuonekana mochwari na baadaye kupotea, bado hawajapata haki ya kuwasitiri ndugu zao kwa heshima."

Mwabukusi amesisitiza kuwa suala la utekaji na kupotea kwa watu linahitaji uchunguzi wa kina na majibu yaliyo wazi. 

"Huwezi kusema watu wanatekwa kimapenzi au kwa sababu za kibinafsi. Mfano Humphrey Polepole, huwezi ukaeleza ni mtu ambaye ameanza mapenzi ukubwani kiasi cha kudanganywa, akafichwa chumbani na hadi leo asimuone mama yake anamtafuta. 

Haya, Mdude Nyagali, ugomvi wa mapenzi yapi? Katika mazingira kama haya tunahitaji majibu ya kina na yenye tafiti," alisema Mwabukusi.

Post a Comment

Previous Post Next Post