Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam chini ya Kamanda SACP Jumanne Muliro limefanikiwa kupata sehemu ya kichwa cha mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), James Rogers Temba, kikiwa kimefukiwa ardhini katika eneo la Kitunda Kibeberu jijini Dar es Salaam, hatua inayotajwa kuwa mafanikio makubwa katika uchunguzi wa tukio hilo lililoitikisa jamii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 13, 2026 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, mabaki hayo yamepatikana baada ya operesheni maalum iliyohusisha uchunguzi wa kina pamoja na matumizi ya mbinu za kisayansi katika kufuatilia wahusika wa tukio hilo la mauaji.
Kamanda Muliro amesema ugunduzi huo umewezesha kukamatwa kwa mganga wa kienyeji anayefahamika kwa jina la Said Ally maarufu kama “Side”, mwenye umri wa miaka 31 na mkazi wa Kitunda, pamoja na watuhumiwa wengine wanne wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo la kinyama lililozua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, sehemu hiyo ya kichwa ilikuwa imefukiwa ardhini na watu wanaotuhumiwa kutekeleza uhalifu huo, huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili kubaini mazingira yote ya tukio pamoja na mtandao mzima wa waliohusika.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabaki hayo yamepatikana ikiwa ni siku kadhaa tangu kupatikana kwa kiwiliwili cha marehemu mnamo Aprili 30 mwaka huu, tukio ambalo lilisababisha mshtuko mkubwa kwa familia, wanafunzi na jamii kwa ujumla kutokana na ukatili wake.

Post a Comment