Mvutano wa kisiasa uliowahi kujitokeza kati ya Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Rwanda, Paul Kagame mwaka 2013, uliibua taharuki kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukihusishwa na msimamo wa Tanzania kuhusu mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na makundi ya waasi wakiwemo M23 pamoja na FDLR.
Chanzo cha mvutano huo kilikuwa ni kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyetoa pendekezo la kidiplomasia kwamba mataifa ya Rwanda, Uganda na DRC yafikirie kufanya mazungumzo na makundi ya waasi ili kupata suluhisho la kudumu la migogoro iliyokuwa ikiendelea katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Kauli hiyo ilitolewa pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa Afrika, ambapo Tanzania ilisisitiza umuhimu wa mazungumzo badala ya kuendelea kwa mapigano.
Hata hivyo, pendekezo hilo halikupokelewa vizuri na Serikali ya Rwanda. Rais Paul Kagame alionyesha kutoridhishwa waziwazi na msimamo huo, akisisitiza kuwa Rwanda haiwezi kufanya mazungumzo na kundi la FDLR ambalo lilihusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Kauli za Kagame zilielezwa kuwa kali na zenye kuashiria hasira dhidi ya ushauri uliotolewa na Rais Kikwete.
Post a Comment