Jamii nchini Uingereza imeachwa katika mshtuko mkubwa baada ya kiongozi wa dini aliyekuwa akiheshimika katika msikiti mmoja wa East London, Abdul Halim Khan, kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kufuatia kupatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono wasichana na wanawake kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mahakama ilieleza kuwa Khan, mwenye umri wa miaka 54, alitumia nafasi yake ya kidini na ushawishi wake ndani ya jamii kuwashawishi wazazi na watoto kuwa alikuwa na uwezo wa kuwaondolea mapepo na roho chafu kupitia kile alichokiita “matibabu maalumu”.

Hata hivyo, nyuma ya madai hayo kulikuwa na mtandao wa vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya waathirika saba, baadhi yao wakiwa na umri mdogo wa miaka 12 pekee.
Mmoja wa manusura, aliyefahamika kwa jina la kubuni la Aria, alisema alipelekwa kwa imam huyo akiwa na miaka 13 baada ya familia yake kuamini angeweza kumsaidia kutokana na matatizo aliyokuwa akipitia.
Badala ya msaada, alijikuta akiingia katika mazingira ya hofu na vitisho ambapo aliaminishwa kuwa familia yake ingeweza kupatwa na mabaya ikiwa angesema ukweli kuhusu yaliyokuwa yakitokea.
Post a Comment