Ridhiwani na mwingine mmoja wafariki dunia kwa ajali ya Gari, Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha vifo vya watu wawili kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika daraja la Wami, Kata ya Mandela, Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani. 

Waliofariki dunia ni Hidaya Mgema Mzireni, mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa Mtoni Kijichi, Dar es Salaam, ambaye alikuwa mfanyakazi wa sekta binafsi na alifariki papo hapo katika eneo la tukio, pamoja na Juma Ridhiwani Juma, mwenye umri wa miaka 35, dereva wa Toyota Hillux na mkazi wa Dar es Salaam, aliyefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Msata.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Msoga, Wilayani Chalinze kwa taratibu za kisheria na kijamii.Ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hillux yenye namba T.937 EHQ na Shacman yenye namba T.316 ENF/T.899 EQT, yaliyogongana uso kwa uso katika barabara kuu ya Dar es Salaam–Morogoro na kusababisha uharibifu mkubwa wa magari pamoja na vifo hivyo. 

Taarifa rasmi iliyotolewa Juni 7, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Juni 6, 2026 majira ya saa 5:45 usiku.

Post a Comment

Previous Post Next Post