Ummy Mwalimu amemshukuru Mwenyezi Mungu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuteuliwa kuwa Mshauri wa Rais kuhusu Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.
Kauli yake iliyojaa shukrani ilitolewa baada ya kupokea uteuzi huo muhimu ambao pia unamfanya kuwa Kinara wa Afya ya Mama na Mtoto wa Umoja wa Afrika (African Union Champion for Maternal and Child Health).
Katika taarifa yake, Ummy Mwalimu aliandika: “ALHAMDULILLAH ALHAMDULILLAH. Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa baraka zake nyingi kwangu.”
Aliendelea kumshukuru Rais Samia kwa kumwamini na kumteua katika wadhifa huo muhimu, akisisitiza kuwa atatekeleza majukumu yake kwa weledi, bidii na uaminifu mkubwa.
“Ahadi yangu kwa Mhe. Rais ni kuwa nitatekeleza majukumu yangu kwa weledi, bidii na uaminifu mkubwa kwake na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” aliandika.
“Ahadi yangu kwa Mhe. Rais ni kuwa nitatekeleza majukumu yangu kwa weledi, bidii na uaminifu mkubwa kwake na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” aliandika.
Aliahidi kutambua heshima kubwa aliyopewa na kuwa mwakilishi bora wa nchi katika ngazi ya Afrika kuhusu afya ya mama na mtoto.
Mwishoni, Ummy Mwalimu aliwashukuru wote walioitoa salamu za pongezi na kumwombea heri. “Asanteni sana. Mwenyezi Mungu awabariki,” aliandika huku akiwa na hisia za furaha na shukrani.
Mwishoni, Ummy Mwalimu aliwashukuru wote walioitoa salamu za pongezi na kumwombea heri. “Asanteni sana. Mwenyezi Mungu awabariki,” aliandika huku akiwa na hisia za furaha na shukrani.
Post a Comment