Kipindi cha Hekaheka ya Clouds FM leo Juni 17,2026 kimetikisa hisia za maelfu ya wananchi baada ya kuanikwa kwa kisa cha kusikitisha kilichomkuta mama mmoja ambaye alinusurika kuuawa na mtu aliyemwamini kama rafiki wa karibu...Tazama video hapa.
Tukio hilo limeibua mjadala mzito kuhusu usalama na tahadhari tunapokutana na watu wapya katika maeneo ya umma hususan hospitalini.
Dada huyo alieleza kwa uchungu namna alivyokutana na mtuhumiwa huyo wakiwa hospitalini.
Katika mazungumzo yao ya awali mtuhumiwa alimwambia dada huyo kuwa anafanana sana na ndugu yake wa karibu hali iliyojenga uaminifu wa haraka.
Urafiki huo uliendelea kukua na baadaye mtuhumiwa alipata fursa ya kujiingiza katika maisha ya mama huyo bila hofu yoyote.
Hata hivyo nia halisi ya mtuhumiwa ilikuwa ovu na yenye hila mbaya. Inadaiwa kuwa lengo kuu la mtu huyo lilikuwa kumuua mama huyo ili aweze kutekeleza mpango wa kumteka na kumuiba mtoto wake mchanga.
Mipango hiyo ilianza kufichuka baada ya vitendo vya mtuhumiwa kuanza kuleta shaka kubwa huku jitihada za kudhuru maisha zikianza kuonekana wazi.

Post a Comment