Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Buluba Mabelele, amezua mjadala mkubwa baada ya kueleza kuwa yupo upande wa kuona Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akiachiwa huru na kurejea uraiani....Tazama video hapa.
Akizungumza katika mahojiano yaliyosambaa mitandaoni, Buluba alisema kuwa pamoja na kuheshimu mamlaka na uhuru wa mahakama kufanya kazi zake, anaamini kuwa suala la Tundu Lissu limekuwa likiipa Tanzania taswira isiyokuwa nzuri mbele ya jamii ya kimataifa.
"Mimi nipo upande wa Tundu Lissu aachiwe huru, arudi uraiani. Haitufundishi mahakama kufanya kazi yake lakini hili suala la Lissu linatuchafua sana kama Taifa," alisema Buluba.
Kauli hiyo imeibua maoni tofauti kutoka kwa wananchi na wadau wa siasa, huku baadhi wakimpongeza kwa kusema kile wanachodai ni hisia za wananchi wengi, na wengine wakisisitiza kuwa mchakato wa kisheria unapaswa kuachwa uendelee bila shinikizo la kisiasa.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaeleza kuwa kauli hiyo ni miongoni mwa matamko machache kutoka kwa kada wa CCM yanayogusia moja kwa moja sakata la Tundu Lissu, jambo linaloongeza uzito wa mjadala unaoendelea kuhusu mustakabali wa siasa za Tanzania na umuhimu wa kulinda taswira ya taifa mbele ya dunia.
Kadri mjadala huo unavyoendelea, macho ya wengi yameelekezwa kwenye hatua zitakazofuata katika kesi inayomkabili Tundu Lissu pamoja na athari zake katika mazingira ya kisiasa nchini.

Post a Comment