Anne Makinda Azungumzia Uzoefu wa Bunge, Afunguka Mazito Kuhusu Lissu

Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, ameibua mjadala baada ya kunukuliwa akizungumzia uzoefu wake wa uongozi bungeni na namna ambavyo baadhi ya wabunge waliwahi kuchangia kuimarisha mijadala ya sheria kwa kutumia hoja zenye weledi mkubwa...............TAZAMA VIDEO HAPA.

Makinda amesema katika vipindi tofauti vya uongozi wake, Bunge lilikuwa likikumbwa na changamoto za mijadala ya miswada na kanuni, lakini lilipata mwelekeo kutokana na mchango wa wabunge waliokuwa na uwezo mkubwa wa uchambuzi wa kisheria na kisera. 

Katika maelezo yake, ametaja mfano wa Mbunge wa zamani Tundu Lissu kama miongoni mwa waliokuwa na mchango mkubwa katika mijadala hiyo.

Ameeleza kuwa mara kadhaa alilazimika kusikiliza kwa makini hoja za wabunge wenye uwezo wa kuchambua sheria ili kusaidia kuondoa mkwamo katika maamuzi ya Bunge, akisisitiza kuwa uongozi wa Bunge unahitaji busara, uvumilivu na uwezo wa kusikiliza mitazamo tofauti.

Post a Comment

Previous Post Next Post