IGP Mahita Atoboa Siri Akitaja Watu Watatu Wanaoamuru Watu Wakamatwe Nchini

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) mstaafu, Omar Mahita, ameibua mjadala mkubwa baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kikatiba unaohusu utoaji wa amri za kukamatwa kwa raia, akisisitiza kuwa si kila kiongozi ana mamlaka ya kutoa maelekezo ya moja kwa moja kwa Jeshi la Polisi................TAZAMA VIDEO.

Akizungumza kupitia mahojiano maalum katika kipindi cha M&S Podcast, Mahita amesema mamlaka ya kutoa maagizo ya kiwango cha juu yanayohusiana na usalama wa nchi na hatua za ukamataji wa watu yanapaswa kutolewa na viongozi wakuu wa Serikali pekee.

Kwa mujibu wa maelezo yake, viongozi hao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, pamoja na Waziri Mkuu. 

Amesema hao ndio wenye mamlaka ya juu ya kisera na kiutendaji ndani ya Serikali, hivyo maelekezo yao ndiyo yanayoweza kuzingatiwa katika masuala ya usalama wa taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post