Mbunge wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima James Mdee, ameibua mjadala mpana wa kisiasa baada ya ujumbe wake wa hivi karibuni kupitia mtandao wa X kuashiria uwezekano wa kurejea katika chama hicho alichowahi kukihudumia kwa muda mrefu kabla ya kuondoka kwake.
Katika ujumbe huo mfupi lakini wenye uzito mkubwa kisiasa, Mdee alisema: “Tulifanya makosa, wengine kwa kujua, wengine kwa bahati mbaya.
Katika ujumbe huo mfupi lakini wenye uzito mkubwa kisiasa, Mdee alisema: “Tulifanya makosa, wengine kwa kujua, wengine kwa bahati mbaya.
Msituhukumu kwa mapito yetu, bali fungueni milango, karibisheni.” Kauli hiyo imezua tafsiri tofauti miongoni mwa wananchi na wadau wa siasa, wengi wakiona kama ishara ya wazi ya kutafuta maridhiano na uwezekano wa kurejea CHADEMA.
Ujumbe huo umeibua hisia tofauti ndani ya jamii ya kisiasa nchini, hasa ukizingatia historia ya Mdee ndani ya CHADEMA na baadaye kuhamia katika mazingira ya kisiasa yaliyosababisha mjadala mkubwa kuhusu uhusiano wake na chama hicho.

Wengine wameona kauli hiyo kama hatua ya kujaribu kufungua ukurasa mpya wa mazungumzo ya kisiasa, huku wengine wakichukulia kama ujumbe wa binafsi usio na uamuzi rasmi wa kisiasa.SOMA ZAIDI.
Post a Comment