Daktari wa India ale mavi ya ng’ombe,adai kwamba husafisha mwili, akili na roho (VIDEO)

Dk Manoj Mittal, mtaalamu wa watoto kutoka Haryana, nchini India, amezua mjadala mkali mtandaoni baada ya kuonekana kwenye kamera akipongeza faida za kula mavi ya ng’ombe, huku akiyala mwenyewe....TIZAMA VIDEO HAPA

Tiba ya jadi ya India kwa muda mrefu imekuwa ikihamasisha mavi ya ng’ombe kama tiba ya kila kitu ambayo inaweza hata kuzuia magonjwa kama saratani na Covid, lakini hii haikujumuisha madaktari waliopata mafunzo ambao kwa kawaida huamini mambo kama sayansi na majaribio ya kitabibu.

Hata hivyo, kama ilivyo karibu katika kila fani, kuna watu wa kipekee, na Manoj Mittal, MD kutoka wilaya ya Karnal huko Haryana, bila shaka ni mmoja wa hao. TIZAMA VIDEO HAPA.Katika video iliyopostiwa hivi karibuni ambayo imeenea sana mtandaoni, Mottal anaonekana akila vipande vya mavi ya ng’ombe na kusifu faida zake kwa mwili wa binadamu, akili na roho.

“Kila sehemu ya Panchagavya inayopatikana kutoka kwa ng’ombe ni ya thamani sana kwa binadamu,” Mittal anasema. “Angalia, tukila mavi ya ng’ombe, basi mwili na akili zetu husafika. Nafsi yetu husafika. Mara tu inapoingia mwilini mwetu, husafisha mwili wetu.”TIZAMA VIDEO HAPA

Daktari huyo wa watoto aliongeza kuwa mama yake alikuwa akifungua mfungo wake kwa kula mavi ya ng’ombe na kwamba wanawake wanaotumia taka hiyo ya ng’ombe hawahitaji tena upasuaji wa kujifungua (cesarean) wakati wa kujifungua.TIZAMA VIDEO HAPA

Katika video hiyo, Dk Manoj Mittal anaonekana akichukua donge la mavi ya ng’ombe na kisha kwa kawaida akila vipande vyake kana kwamba ni mkate.

Kitendo chake kimepokea maoni mseto kwenye mitandao ya kijamii, ambapo kundi moja la watu likimsifu kwa kukumbatia tiba ya jadi ya India, na wengine wakimkosoa kwa kuacha mantiki ya kisayansi ili kueneza “wazimu huu.”TIZAMA VIDEO HAPA

“Mamlaka ya tiba ya India inapaswa kuchukua hatua kuhusu hili na kufuta leseni yake ya kufanya kazi ya udaktari. Kama daktari wa watoto, hapaswi kuagiza gobar kwa watoto wadogo wasio na hatia,” mtumiaji mmoja wa Facebook aliandika.

Post a Comment

Previous Post Next Post