Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amesema moja ya makosa makubwa yaliyofanyika nchini ni kuruhusu wafanyabiashara kuwa sehemu kubwa ya uamuzi wa kisiasa, akidai hali hiyo imebadili mwelekeo wa maamuzi mengi ya umma.S.O.M.A Z.AI.DI.
Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa na vyombo vya habari, Profesa Assad alisema kuwa wakati wa uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, kulikuwa na mipaka iliyoweka wazi tofauti kati ya masuala ya biashara na siasa, jambo lililosaidia kulinda maslahi ya wananchi.
Kwa mujibu wa Assad, mfanyabiashara anapoingia katika nafasi za maamuzi ya kisiasa kuna uwezekano wa baadhi ya maamuzi kuelekezwa zaidi kwenye manufaa binafsi badala ya maslahi mapana ya taifa.
Alieleza kuwa changamoto hiyo imekuwa ikijitokeza katika mataifa mbalimbali duniani ambapo nguvu ya fedha huanza kuwa na ushawishi mkubwa katika mchakato wa kisiasa na kufanya maamuzi ya umma kuonekana yanawanufaisha wachache kuliko wengi.
Post a Comment