Chifu Songea Mbano wa Songea ameeleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, hana hadhi ya kuwa Chifu, akisema tukio la kumvalisha mavazi ya uchifu lililofanyika Songea halikufuata taratibu za kimila.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mzee Mbano amesema mtu aliyemvalisha Heche mavazi hayo ni kijana ambaye si sehemu ya mamlaka rasmi za kimila, bali ni msanii anayefahamika kwa jina la Lucius Joseph Ponela.
Kwa mujibu wa Mzee huyo, kijana huyo ni msanii wa kikundi cha Ligiu na hakupaswa kufanya tukio la kumvisha Heche mavazi ya kichifu, akisisitiza kuwa hatua hiyo ilikuwa kinyume na taratibu na mila za Wangoni.S.O.M.A Z.A
Post a Comment