Washington / Tehran – Serikali ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimekubaliana kuheshimu mamlaka, mipaka na uhuru wa kila upande, pamoja na kujizuia kuingilia mambo ya ndani ya nchi husika, ikiwa ni sehemu ya makubaliano mapya ya kusitisha mapigano kati ya mataifa hayo mawili...TAZAMA VIDEO.
Kwa mujibu wa taarifa za pande zote, makubaliano hayo yanaonekana kufungua ukurasa mpya katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya Washington na Tehran, ambao kwa muda mrefu umekuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi.
Hata hivyo, licha ya hatua hiyo kuchukuliwa kama ishara ya kupungua kwa uhasama, bado kuna mashaka kuhusu namna makubaliano hayo yatakavyopokelewa ndani ya Iran, hususan kutoka kwa makundi yanayopinga serikali ya nchi hiyo na yanayodai mabadiliko ya kisiasa.

Kwa upande mwingine, wakati wa maandamano ya raia wa Iran yaliyotokea mapema mwaka huu kupinga utawala wa nchi yao, Marekani iliripotiwa kutoa ahadi za kuunga mkono waandamanaji hao. Hata hivyo, hadi sasa hakuna hatua za moja kwa moja zilizoshuhudiwa kutekelezwa kuhusiana na ahadi hizo, jambo ambalo limeibua maswali miongoni mwa baadhi ya wachambuzi kuhusu uhalisia wa sera hizo za nje.
Wakati uhusiano kati ya mataifa hayo ukijaribiwa kurekebishwa kupitia makubaliano haya mapya, macho ya dunia yanaelekezwa Tehran na Washington kuona kama pande zote zitatekeleza kwa vitendo ahadi zilizowekwa na kama hatua hiyo inaweza kuleta utulivu wa kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.
Post a Comment