IGP Wambura Azua Gumzo Baada ya Kutoa Kauli Hii Kuhusu Sakata la Polisi Dhidi ya Wananchi

Kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Wambura, kwamba polisi na wananchi si makundi mawili yanayopingana bali ni sehemu ya jamii moja inayotegemeana, imezua mjadala na kuvuta hisia za wengi wakati ambapo kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusu uhusiano kati ya vyombo vya usalama na wananchi nchini.

IGP Wambura alitoa kauli hiyo leo Ijumaa, Juni 5, 2026, mkoani Mara wakati akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya askari polisi katika Mkoa wa Tarime-Rorya. 

Akizungumza mbele ya viongozi wa serikali, jeshi la polisi na wananchi waliohudhuria hafla hiyo, alisema mafanikio ya kulinda usalama wa nchi hayawezi kupatikana bila ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na jeshi la polisi.

Katika maelezo yake, IGP Wambura alisisitiza kuwa askari polisi ni sehemu ya wananchi na wanaishi ndani ya jamii wanayoihudumia, jambo linalofanya ushirikiano kuwa msingi muhimu wa kuimarisha usalama. 

Alieleza kuwa mradi wa nyumba za kisasa za makazi ya askari uliofanikiwa Tarime-Rorya ni mfano halisi wa jinsi wananchi wanavyoweza kushirikiana na jeshi hilo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili askari.

Post a Comment

Previous Post Next Post