Mbunge Erik Shigongo Aguswa na Ujasiri wa Mama Aliyemwokoa Kijana Mikononi Mwa Wananchi Wenye Hasira

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, ameonyesha kuguswa na kitendo cha kishujaa cha mama mmoja aliyemkingia kifua kijana aliyekuwa akishambuliwa na wananchi baada ya kutuhumiwa kuhusika katika wizi wa simu.

Tukio hilo lilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kupitia video iliyomuonyesha mama huyo akisimama mbele ya kijana huyo na kuwazuia wananchi waliokuwa na hasira wasimdhuru. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa, kijana huyo alikuwa akituhumiwa kuiba simu pamoja na mwenzake ambaye alifanikiwa kutoroka eneo la tukio. 

Hata hivyo, pikipiki iliyokuwa ikihusishwa na tukio hilo ilichomwa moto na wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post