Iran Yaidungua tena drone ya Marekani

Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kuongezeka baada ya taarifa mpya kudai kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limefanikiwa kuidungua tena drone ya Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi...............TAZAMA VIDEO HAPA.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea takribani saa moja iliyopita huku likizua hofu mpya ya kuzuka kwa mapigano makubwa zaidi katika Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vya Iran, drone hiyo aina ya MQ-9 Reaper ilidaiwa kuingia katika anga ambalo Tehran inaliona kuwa ni eneo lake la kijeshi kabla ya kushambuliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya IRGC. Iran imesema hatua hiyo ilikuwa ya kujilinda dhidi ya kile ilichokiita “uchokozi wa Marekani.”

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo tayari Marekani na Iran zimekuwa katika mvutano mkali kuhusu usalama wa Bahari ya Hormuz, eneo muhimu sana kwa usafirishaji wa mafuta duniani. 

Katika siku za hivi karibuni, Marekani imekuwa ikidai kuwa Iran inatishia usalama wa meli za biashara huku Iran nayo ikiishutumu Washington kwa kufanya mashambulizi na kupeleka vifaa vya kijeshi karibu na mipaka yake.

IRGC pia imedai kuwa mbali na kuidungua drone hiyo, iliweza kulazimisha ndege nyingine za Marekani kuondoka katika eneo hilo. 

Marekani bado haijatoa tamko rasmi kuthibitisha au kukanusha tukio hilo, jambo ambalo limeongeza sintofahamu kuhusu kilichotokea hasa angani katika Ghuba ya Uajemi.

Post a Comment

Previous Post Next Post