Marekani Yaishambulia Iran Tena na Makombora Haya Mazito sababu ni Hii hapa

Taarifa mpya kutoka Jeshi la Marekani kupitia United States Central Command zinaeleza kuwa vikosi vyao vimedungua ndege nne zisizo na rubani (drones) za Iran zilizokuwa zikielekea eneo la Mlango Bahari wa Strait of Hormuz, wakidai kuwa zilikuwa tishio la moja kwa moja kwa usalama wa meli zinazopita katika njia hiyo muhimu ya kimataifa. ..................TAZAMA VIDEO.

Eneo la Hormuz linachukuliwa kuwa moja ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani, ambapo sehemu kubwa ya mafuta yanayotoka mataifa ya Ghuba ya Uajemi hupitia kabla ya kufika katika masoko mbalimbali ya dunia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua ya kudungua ndege hizo ilifanyika baada ya Marekani kubaini kuwa zilikuwa zikifanya shughuli ambazo zingeweza kuhatarisha usalama wa usafiri wa majini pamoja na maslahi ya mataifa washirika wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi. 

Baada ya operesheni hiyo, CENTCOM ilisema vikosi vyake vilianzisha mashambulizi ya kulipiza na kulenga vituo vya rada vya Iran vilivyopo katika eneo la Goruk pamoja na Qeshm Island.

Jeshi la Marekani limesema mashambulizi hayo yalikuwa na lengo la kupunguza uwezo wa Iran kufuatilia na kuelekeza mashambulizi dhidi ya meli na vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo hilo. 

Kwa mtazamo wa Marekani, kuharibu miundombinu ya rada kunasaidia kuzuia mashambulizi zaidi na kulinda usalama wa vikosi vyake pamoja na washirika wake wa kikanda.

Post a Comment

Previous Post Next Post