Jeshi la Israel limetoa agizo jipya la dharura la kuwataka wakazi wa mji wa Tyre, ulioko kusini mwa Lebanon, kuondoka mara moja katika makazi yao.
Hatua hii imeibua taharuki kubwa miongoni mwa raia na wadau wa kimataifa, ikionyesha kuendelea kwa hali tete ya usalama katika eneo hilo.
Kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa X, msemaji wa jeshi la Israel alieleza kuwa agizo hilo linawahusu pia wakazi wa maeneo ya jirani, ikiwemo kambi za Al-Bas na Zakuk al-Mufdi.
Ujumbe huo ulisema wazi: “Lazima muondoke katika nyumba zenu mara moja na kuelekea kaskazini mwa Mto Zahrani.”
Ujumbe huo ulisema wazi: “Lazima muondoke katika nyumba zenu mara moja na kuelekea kaskazini mwa Mto Zahrani.”
Tangu kuanza kwa mashambulizi ya anga na operesheni za kijeshi za Israel kusini mwa Lebanon mwezi Machi, mamia ya maelfu ya raia wa Lebanon wamelazimika kuyahama makazi yao.
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yameonya kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka kwa kasi, na hali ya kibinadamu imezidi kuwa mbaya kutokana na ukosefu wa huduma za msingi kama vile chakula, maji safi na huduma za afya.
Wachambuzi wa usalama wa kikanda wanasema agizo hilii na huduma za afya.Wachambuzi wa usalama wa kikanda wanasema agizo hili jipya linaashiria uwezekano wa operesheni kubwa zaidi ya kijeshi, jambo linaloweza kuongeza mvutano kati ya Israel na Hizbullah.

Serikali ya Lebanon haijatoa tamko rasmi kufuatia agizo hilo, lakini wadau wa kisiasa wanaonya kuwa hatua ya Israel inaweza kuathiri juhudi za kidiplomasia zinazolenga kupunguza mapigano na kurejesha utulivu.
Kwa upande wa raia, hofu imeenea katika mji wa Tyre na maeneo ya jirani, huku familia zikihangaika kutafuta njia salama za kuondoka.
Mashirika ya misaada yameanza kujiandaa kutoa msaada wa dharura kwa wakimbizi wapya watakaofika kaskazini mwa Mto Zahrani. SOMA ZAIDI.
Post a Comment