Mvutano kati ya Marekani na Iran umeingia hatua mpya ya hatari kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya pande zote mbili yaliyoripotiwa katika eneo la Ghuba ya Uajemi, hali inayozua hofu kubwa kuhusu usalama wa kimataifa na uthabiti wa soko la nishati duniani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani CENTCOM, jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi ya kujihami dhidi ya malengo ya kijeshi ya Iran katika Kisiwa cha Qeshm, kilicho karibu na Mlango wa Hormuz.

Operesheni hiyo ililenga kituo cha udhibiti wa kijeshi cha Iran kinachodaiwa kuhusika na urushaji wa makombora ya masafa marefu pamoja na droni kuelekea mataifa ya Ghuba na maeneo yenye maslahi ya Marekani.
CENTCOM ilieleza kuwa Iran ilirusha makombora kadhaa kuelekea maeneo ya Kuwait na Bahrain, ambapo baadhi ya makombora hayo yalishindwa kufika yalipokusudiwa.
CENTCOM ilieleza kuwa Iran ilirusha makombora kadhaa kuelekea maeneo ya Kuwait na Bahrain, ambapo baadhi ya makombora hayo yalishindwa kufika yalipokusudiwa.
Kulingana na taarifa hizo, makombora mawili yaliyolenga Kuwait yalizimwa kabla ya kufika, huku mengine matatu yaliyolenga Bahrain yakidunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya pamoja kati ya Marekani na Bahrain. SOMA ZAIDI.
Post a Comment