Pigo Kubwa kwa Iran na Marekani Baada ya Tukio Jipya la Mashambulizi Yanayozidi Kutikisa Ghuba ya Uajemi

Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kushika kasi baada ya tukio jipya la mashambulizi ya kijeshi kuripotiwa katika eneo la Ghuba ya Uajemi, hali inayozidisha wasiwasi wa usalama wa kikanda na kuibua hofu kuhusu athari zake kwa uchumi wa dunia, hususan sekta ya nishati.

TAZAMA VIDEO.  

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani CENTCOM, vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi ya kujihami dhidi ya malengo ya kijeshi ya Iran katika Kisiwa cha Qeshm kilicho karibu na Mlango wa Hormuz. 

Operesheni hiyo ilielekezwa katika kituo cha udhibiti wa kijeshi kinachodaiwa kuratibu mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya maeneo ya kimkakati ya Marekani na washirika wake katika eneo la Ghuba.

CENTCOM ilieleza kuwa Iran ilianzisha mashambulizi mapya kwa kurusha makombora kadhaa kuelekea Kuwait na Bahrain. 

Kulingana na taarifa hizo, makombora mawili yaliyolenga Kuwait yalishindwa kufika yalipokusudiwa baada ya kukabiliwa na hitilafu au kuzimwa mapema, huku makombora mengine matatu yaliyolenga Bahrain yakidunguliwa na mifumo ya pamoja ya ulinzi wa anga kati ya vikosi vya Marekani na Bahrain.

Post a Comment

Previous Post Next Post