Makonda Awageuka CCM Amtaja Adui Wao Mkubwa Hadharani Na Kusema Sio CHADEMA

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema kuwa changamoto kubwa inayoweza kukiangusha chama hicho si vyama vya upinzani kama CHADEMA, bali ni baadhi ya wanachama wa CCM wenyewe wanaotanguliza maslahi binafsi badala ya kuwatumikia wananchi. 

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wanachama na wafuasi wa chama hicho, ambapo alisisitiza umuhimu wa viongozi wa CCM kurejea kwa wananchi na kutatua matatizo yao kwa vitendo.

Makonda alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na mtazamo wa kuamini kuwa upinzani ndio tishio kubwa kwa CCM, lakini ukweli ni kwamba baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho wamekuwa wakichangia kuporomoka kwa imani ya wananchi kutokana na vitendo vya ubinafsi, kutowajibika na kushindwa kusikiliza kero za wananchi.

Katika hotuba yake, Makonda alieleza kuwa chama tawala kina nguvu kubwa kutokana na historia yake na mchango wake katika maendeleo ya taifa, lakini nguvu hiyo inaweza kupungua ikiwa viongozi wake hawataweka mbele maslahi ya wananchi. 

Alisema wananchi wanahitaji kuona matokeo ya ahadi zinazotolewa na viongozi wao badala ya maneno matupu ya kisiasa. SOMA ZAIDI.



Post a Comment

Previous Post Next Post