Rais Samia Asema Kelele Sasa Basi, Achukua Uamuzi Huu Mgumu kwa Faida ya Taifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ni wakati wa kuacha kelele na mijadala isiyo na tija na badala yake kuelekeza nguvu katika utekelezaji wa mikakati ya maendeleo itakayowanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imekuja wakati wa ziara ya kihistoria ya Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, nchini Tanzania, ambapo mataifa hayo mawili yamefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji.

Akizungumza baada ya mazungumzo ya uwili yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Samia alisema Tanzania imeamua kuchukua maamuzi magumu lakini yenye manufaa ya muda mrefu kwa taifa, ikiwemo kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kukuza uchumi wa kidigitali na kuwawezesha vijana kupitia elimu, ujasiriamali na ubunifu.

Katika hatua ya kuonyesha dhamira hiyo, Tanzania na Singapore zilisaini rasimu ya mikataba na hati tano za makubaliano ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali, ikiwemo masuala ya kodi, biashara, uwekezaji, maendeleo ya ujuzi na diplomasia.

Post a Comment

Previous Post Next Post