Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, ambaye alifukuzwa uanachama wa chama hicho mwaka 2020 pamoja na wabunge wengine 18 wa Viti Maalum, amerejea rasmi ndani ya chama hicho baada ya takribani miaka sita tangu kuondoka kwake.......................TAZAMA VIDEO HAPA.
Taarifa ya kurejea kwa Mdee imetolewa leo Juni 7, 2026 na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, kupitia ujumbe aliochapisha kwenye mitandao ya kijamii akithibitisha hatua hiyo. Katika taarifa hiyo, chama kimeeleza kuridhishwa na hatua ya Mdee ya kurejea na kushiriki katika shughuli za chama.
Halima Mdee alikuwa miongoni mwa wabunge wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama kufuatia mvutano ulioibuka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, ambapo CHADEMA ilidai wabunge hao hawakuteuliwa na chama kushika nafasi hizo. Uamuzi huo ulizua mjadala mkubwa ndani na nje ya chama.
Kurejea kwa Mdee kunatajwa kuwa hatua muhimu ndani ya chama hicho kuelekea maandalizi ya shughuli zake za kisiasa na uchaguzi mkuu ujao.

Taarifa ilisema kuwa Mdee ameonesha nia ya kushirikiana na uongozi wa chama ili kuimarisha umoja na nguvu ya CHADEMA katika kanda mbalimbali.
Post a Comment