Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekanusha vikali madai yanayoendelea kusambazwa kwamba Tanzania ipo chini ya vikwazo vya kimataifa.
Kauli hiyo ameitoa akiwa katika ziara yake rasmi nchini Urusi, akisisitiza kuwa taifa linaendelea kuwa huru na linafanya juhudi mbalimbali za kuimarisha maendeleo ya wananchi wake bila kuzuiwa na vikwazo vya aina yoyote.
Akizungumza mbele ya viongozi na wadau mbalimbali wakati wa ziara hiyo, Rais Samia alisema kuwa Tanzania haijawekewa vikwazo vya kiuchumi wala kisiasa vinavyoweza kuathiri shughuli za maendeleo ya nchi.

Alieleza kuwa serikali yake inaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani katika nyanja za biashara, uwekezaji, teknolojia na maendeleo ya kijamii kwa manufaa ya Watanzania.
Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na mjadala mkubwa kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na baadhi ya mataifa ya Magharibi dhidi ya maafisa wa Tanzania wanaotuhumiwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hali hiyo imeibua tafsiri tofauti miongoni mwa wananchi na wachambuzi wa masuala ya siasa, ambapo baadhi walidai kuwa hatua hizo zinaashiria kuwepo kwa vikwazo dhidi ya Tanzania. SOMA ZAIDI.
Post a Comment