Maduka Yavunjwa, Wananchi Wapigwa: ACT Wazalendo Yatoa Tuhuma Nzito Dhidi Ya Polisi Shinyanga

Chama cha ACT Wazalendo kimekilaumu hadharani Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kikidai wanashirikiana kutumia nguvu ya vyombo vya dola kuwakamata na kuwatesa wananchi kwa sababu tu ya msimamo wa kuipinga CCM na viongozi wake............TAZAMA VIDEO HAPA.

Katika taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo Jumamosi, Juni 6, 2026, na Naibu Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi wa chama hicho, Mbarala Maharagande, imeelezwa kuwa hadi sasa jumla ya wananchi 52, wakiwemo wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo, wamekamatwa katika Kata za Idukilo (Kishapu) na Iyabukande (Itwangi).

​Tuhuma hiyo nzito inasema kuwa oparesheni hiyo inalenga kuwakomoa na kuwalazimisha wananchi kuwakubali madiwani wa CCM waliopatikana kwa njia zisizo halali, pamoja na kuwanyamazisha wale wanaofanya ujasiri wa kuhoji taarifa za mapato na matumizi ya kata zao.





Post a Comment

Previous Post Next Post