Meneja wa klabu ya Manchester City, Manchester City Pep Guardiola, amezua mjadala mkubwa katika ulimwengu wa soka baada ya kutoa sifa nzito kwa mfumo wa uchezaji wa FC Barcelona chini ya kocha Hansi Flick, akisisitiza kuvutiwa kwake na mwelekeo wa timu hiyo pamoja na mchango mkubwa wa akademi ya La Masia.........................TAZAMA VIDEO HAPA.
Akizungumza katika mahojiano yaliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari za michezo, Guardiola alieleza wazi kuwa Barcelona ya sasa inamvutia sana kutokana na jinsi inavyocheza soka la kuvutia na la kisasa, huku ikitumia idadi kubwa ya wachezaji waliokulia ndani ya mfumo wa klabu hiyo.
Mimi ni shabiki mkubwa wa Barcelona ya Hansi Flick. Wanacheza soka zuri sana na ni jambo la kushangaza kuona walichokifanya kwa kutumia wachezaji wengi kutoka La Masia alinukuliwa Guardiola akisema.
Kauli hiyo imeibua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa soka duniani, hasa ikizingatiwa historia ya Guardiola ndani ya Barcelona kama mchezaji na baadaye kocha aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa, akijenga enzi ya mafanikio kwa kutumia vipaji vilivyotokana na La Masia.
Kwa mujibu wa Guardiola, mafanikio ya Barcelona chini ya Flick hayawezi kutenganishwa na uamuzi wa klabu kuendelea kuamini vijana wake wa akademi. Amesema kuwa mfumo huo ndiyo unaoipa Barcelona utambulisho wa kipekee katika soka la kisasa.SOMA ZAIDI.

Post a Comment