Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewahi kujibu kwa ukali tuhuma zilizokuwa zikisambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya mijadala ya kisiasa zikimhusisha yeye na mtoto wake, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Tuhuma hizo zilidai kuwa Rais huyo wa zamani alihusika kumsaidia mwanawe baada ya kukamatwa kwa madai ya kuhusishwa na masuala ya dawa za kulevya akiwa nje ya nchi, jambo ambalo Kikwete amelikanusha vikali na kulielezea kama uzushi usio na msingi.
Akizungumza katika mkutano na Watanzania wanaoishi Marekani, uliofanyika katika Hoteli ya Marriott Washington, mjini Washington D.C., Kikwete alitumia lugha kali kueleza msimamo wake kuhusu madai hayo, akisisitiza kuwa hayana ukweli na yanapaswa kupuuzwa na jamii.

Alieleza kuwa nafasi ya Urais ni taasisi nyeti inayohitaji heshima na umakini, hivyo hawezi kujiingiza katika mijadala ya mitaani inayolenga kumchafulia jina yeye binafsi na familia yake.
“This is nonsense – ni mkusanyiko wa upuuzi. Sina muda wala siwezi kupoteza nguvu yangu kujadili upuuzi na ujinga wa namna hiyo,” alinukuliwa Kikwete akisema, kauli ambayo ilizua hisia tofauti miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia hotuba hiyo. SOMA ZAIDI.

Post a Comment