WASHINGTON — Rais wa Marekani Donald Trump amesema amefanikiwa kuzuia hatua ya kijeshi ya Israel kuelekea mji mkuu wa Lebanon, Beirut, huku akisisitiza kuwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran bado yanaendelea licha ya Tehran kutangaza kusitisha mawasiliano kupitia wapatanishi.TAZAMA VIDEO.
Katika siku iliyoshuhudia matukio ya haraka na kauli zinazokinzana kutoka pande mbalimbali za mzozo wa Mashariki ya Kati, Trump alisema mazungumzo aliyofanya na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na mawasiliano na Hezbollah yalisaidia kupunguza hatari ya kuongezeka kwa mapigano nchini Lebanon.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye jukwaa lake la Truth Social Jumatatu, Trump alisema hakuna wanajeshi wa Israel watakaoelekea Beirut na kwamba vikosi vyovyote vilivyokuwa vinaelekea huko tayari vimeagizwa kurejea nyuma.
“Hakutakuwa na wanajeshi wanaoelekea Beirut, na wale waliokuwa njiani tayari wamerudishwa,” alisema Trump.
Rais huyo pia alidai kuwa amekuwa na mazungumzo mazuri na Hezbollah, ambayo yalisababisha makubaliano ya kusitisha mashambulizi kati ya kundi hilo na Israel.
“Walikubaliana kuwa mashambulizi yote yatasimama. Israel haitawashambulia wao, na wao hawataishambulia Israel,” alisema.
Kauli za Trump zilikuja saa chache baada ya Shirika la Habari la Tasnim la Iran, ambalo lina uhusiano wa karibu na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kuripoti kuwa Tehran imeamua kusitisha kubadilishana ujumbe na Marekani kuhusu makubaliano ya amani kutokana na operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel nchini Lebanon.
Ripoti hiyo pia ilieleza kuwa Iran imeazimia kuzuia kikamilifu shughuli katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, moja ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani, na kuongeza maeneo ya mapambano ikiwa hali itaendelea kuzorota.
Hata hivyo, tofauti na matamshi yake ya kawaida ya ukali, Trump alionekana kupunguza uzito wa taarifa hizo.

Alipoulizwa kuhusu hatua ya Iran, alisema Washington haikupokea taarifa rasmi kutoka Tehran kuhusu kusitishwa kwa mazungumzo hayo.
“Sijali kama mazungumzo yamekwisha au la. Kwa kweli sijali,” alisema Trump katika mahojiano na vyombo vya habari vya Marekani.
Licha ya kauli hiyo, alionyesha kuwa bado yuko tayari kuendeleza juhudi za kidiplomasia, akisema kuwa kusitishwa kwa mazungumzo hakumaanishi kuwa Marekani itaanza mashambulizi mapya dhidi ya Iran.
“Haimaanishi kwamba tutaenda na kuanza kurusha mabomu kila mahali. Tutaendelea na hatua zetu za kuzuia,” alisema.
Trump pia alitumia ujumbe mwingine kwenye Truth Social kusisitiza kuwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran yanaendelea kwa kasi kubwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika siku za karibuni.
Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilitoa taarifa kali ikiilaumu Marekani kwa kushindwa kuizuia Israel kuendelea na mashambulizi dhidi ya Lebanon.

Tehran ilisema kuwa Washington ina jukumu la moja kwa moja katika ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa yamefikiwa hapo awali.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, Marekani inawajibika sio tu kwa ukiukaji wa makubaliano dhidi ya Iran bali pia kwa mashambulizi yanayofanywa na Israel nchini Lebanon.
“Jukumu la moja kwa moja la Marekani katika ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano dhidi ya Iran na ukiukaji unaofanywa na utawala wa Israel dhidi ya Lebanon ni dhahiri,” ilisema taarifa hiyo.
Iran iliongeza kuwa itatumia uwezo wake wote wa kijeshi na kisiasa kulinda maslahi yake popote itakapoona ni muhimu kufanya hivyo.
Kauli hizo ziliungwa mkono na maafisa waandamizi wa kijeshi wa Iran waliyonukuliwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo wakisema kuwa Tehran iko tayari kuchukua hatua mpya za kujihami, ikiwemo kufungua maeneo mapya ya mapambano na kudumisha ushawishi wake katika Mlango wa Hormuz.
Mshauri wa Kiongozi Mkuu wa Iran na kamanda wa zamani wa IRGC, Mohsen Rezaei, pia alionya kuwa Iran haitakubali kuendelea kwa kile alichokiita mzingiro wa baharini wala kuongezeka kwa mvutano nchini Lebanon.
“Hatutaruhusu kuendelea kwa mzingiro wa baharini, na pia hatutavumilia kuongezeka kwa mvutano nchini Lebanon,” alisema kupitia mtandao wa X.
Aliongeza kuwa uvumilivu wa vikosi vya jeshi vya Iran una mipaka na kwamba Tehran iko tayari kujibu hatua zozote itakazoona zinahatarisha usalama wake wa kitaifa.
Kadri hali inavyoendelea kubadilika kwa kasi, juhudi za kidiplomasia za Marekani zinakabiliwa na mtihani mkubwa.

Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaonya kuwa kushindwa kwa mazungumzo kati ya Washington na Tehran pamoja na kuongezeka kwa mapigano nchini Lebanon kunaweza kusababisha mzozo mkubwa zaidi wa kikanda, wenye athari kwa usalama wa dunia na soko la kimataifa la nishati.
Kwa sasa, dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu hatua zinazochukuliwa na Marekani, Iran, Israel na Hezbollah huku matumaini ya kurejea kwa utulivu yakibaki kutegemea mafanikio ya diplomasia kuliko nguvu za kijeshi.

Post a Comment