Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon hayakufanyika kwa ushirikiano wa Marekani na kwamba Washington haikuhusika kwa namna yoyote katika operesheni hiyo.
Ameeleza kuwa serikali yake haikuridhishwa na hatua hiyo na imeonyesha kutofurahishwa na namna tukio hilo lilivyotekelezwa.
Trump alibainisha kuwa baada ya mashambulizi hayo, Iran ilijibu kwa kurusha makombora kuelekea Israel usiku huo, jambo lililoongeza hofu ya kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Trump alibainisha kuwa baada ya mashambulizi hayo, Iran ilijibu kwa kurusha makombora kuelekea Israel usiku huo, jambo lililoongeza hofu ya kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, alisema kuwa licha ya hatua hiyo ya Iran, anaamini bado kuna nafasi ya kutafuta suluhisho la kidiplomasia badala ya kuendelea na mzunguko wa mashambulizi na kulipizana kisasi.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Trump alisema ana mpango wa kuwasiliana moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ili kumshawishi kuepuka kujibu mashambulizi ya Iran kwa hatua nyingine za kijeshi.

Kwa mujibu wake, kujibu mashambulizi hayo kunaweza kusababisha mzozo huo kuendelea na kuzidi kuwa mgumu kudhibiti.
Trump alisisitiza kuwa lengo lake ni kuona pande zote zikionyesha uvumilivu na kutoa nafasi kwa juhudi za mazungumzo na diplomasia.
Trump alisisitiza kuwa lengo lake ni kuona pande zote zikionyesha uvumilivu na kutoa nafasi kwa juhudi za mazungumzo na diplomasia.
Alieleza kuwa iwapo Israel itachagua kujibu kwa mashambulizi mapya, hali inaweza kugeuka kuwa mbaya zaidi na kuharibu jitihada zinazofanyika za kufikia makubaliano ya amani katika eneo hilo.
Post a Comment