Washington, Marekani — Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametoa kauli kali na yenye uzito mkubwa kuhusu mustakabali wa uhusiano kati ya Israel na Iran, akisema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hatakuwa na chaguo lingine zaidi ya kukubali makubaliano yoyote yatakayofikiwa kati ya Marekani na Iran.
Akizungumza kupitia simu na gazeti la Financial Times, Trump alisisitiza kuwa nafasi ya Israel katika mazungumzo hayo ni finyu, akidai kuwa uamuzi wa mwisho unategemea Marekani.
Yeye hatakuwa na jinsi. Mimi ndiye ninayeamua. Mimi ndiye ninayeamua kila kitu. Yeye (Netanyahu) si anayeamua Trump alinukuliwa akisema katika mazungumzo hayo.
Kauli hiyo imezua mjadala mpana wa kisiasa kuhusu ushawishi wa Washington katika masuala ya Mashariki ya Kati, hasa katika muktadha wa mvutano unaoendelea kati ya Israel na Iran.
Kwa mujibu wa taarifa za Financial Times Financial Times, Trump alisisitiza kuwa mashambulizi ya hivi karibuni kati ya pande hizo hayajabadilisha msimamo wake kuhusu mchakato wa mazungumzo ya makubaliano.
Tutaona jinsi itakavyomalizika alisema Trump akitoa kauli inayoacha mlango wazi kwa maendeleo zaidi ya kidiplomasia.
Aidha, Trump alinukuliwa pia na Axios Axios akisema kuwa atamuomba Netanyahu asiendelee na hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Iran, ili kuwezesha nafasi ya kufanikisha makubaliano ya pande tatu—Marekani, Israel na Iran.
Kauli hizi zimekuja katika kipindi ambacho hali ya Mashariki ya Kati bado ni tete, huku jitihada za kidiplomasia zikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu ya mzozo kati ya Israel na Iran.
Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema kauli ya Trump inaweza kuongeza shinikizo la kisiasa ndani ya Israel, lakini pia huenda ikaibua mjadala mpya kuhusu kiwango cha ushawishi wa Marekani katika maamuzi ya usalama wa kikanda.

Post a Comment