Trump Yahamisha Ndege Zake Kutoka Israel Huku Hofu ya Kuongezeka kwa Mvutano wa Kieneo Ikiongezeka

Serikali ya Marekani imeanza utekelezaji wa mpango wa kuhamisha baadhi ya ndege zake zilizokuwa zimetumwa nchini Israel kwenda katika vituo vya kijeshi vilivyoko barani Ulaya, hatua inayokuja wakati mvutano wa usalama katika Mashariki ya Kati ukiendelea kuzua wasiwasi miongoni mwa mataifa mbalimbali duniani......................................TAZAMA VIDEO.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, operesheni hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya muda wa saa 72. 

Ndege hizo zinadaiwa kuondolewa kutoka katika vituo tofauti vya kijeshi nchini Israel na kupelekwa katika maeneo salama zaidi ambayo yanaweza kutumika kwa haraka iwapo hali ya usalama itabadilika ghafla.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya maandalizi ya kijeshi ya Marekani yanayolenga kulinda mali zake za anga huku zikibaki tayari kwa matumizi ya haraka ikiwa kutatokea ongezeko la mashambulizi au mzozo wa moja kwa moja katika eneo hilo. 

Marekani imekuwa mshirika wa karibu wa Israel kwa muda mrefu, jambo linaloifanya kufuatilia kwa karibu maendeleo yote ya kiusalama yanayotokea katika Mashariki ya Kati.

Post a Comment

Previous Post Next Post